Waziri Kiongozi wa Uskochi, Nicola Sturgeon, amesema bunge la Scotland linaweza kupiga kura kuzuwia Uingereza kutoka katika Umoja wa Ulaya.

Anaamini, kikatiba, Uskochi lazima itoe idhini piya, kwamba Uingereza inaweza kumaliza uanachama wake katika EU na yeye atawasihi wabunge wa Scotland kutumia haki yao hiyo.

Uskochi ilipiga kura kwa wingi kubaki katika umoja huo

Bibi Sturgeon alisema, anataka kuwalinda watu wa Scotland na matokeo mabaya na ambayo yatawaumiza, nchi itapotoka katika Umoja wa Ulaya

Ameshazungumza juu ya uwezekano wa kufanya kura nyengine ya maoni, kujitenga na Uingereza

YANGA Mkiwagusa Azam TV Siku ya Mechi Yenu na TP Mazembe Mtakiona Cha Moto-TFF
Mabaki yanayokisiwa kuwa ya ndege ya Malaysia yapatikana TZ