Rais wa Shirikisho la Soka visiwani Zanzibar (ZFF) Seif Kombo Pandu, ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ndani ya shirikisho hilo.

Kombo ameandika barua hiyo pasina kueleza sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake, na badala yake ameandika kuwa hajashurutishwa na mtu yoyote kufanya hivyo.

Hata hivyo ni dhahir inafahamika kuwa Pandu aliwahi kuwa na mikwaruzano na baadhi ya wadau wa soka visiwani humo, na kufikia hatua ya kusimamishwa kwa muda, kabla ya kurudishwa kuendelea na shughuli zake kama kongozi wa ZFF.

No photo description available.
Mwili wa Maalim Seif wawasili Zanzibar, kuzikwa leo
Televisheni yafungiwa kwa kukiuka taratibu za maombolezo