Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewataka wabunge wote kuwasilisha taarifa za mali wanazomiliki kwa Katibu wa Bunge kabla ya Juni 25, 2018.

Taarifa hiyo ya Sekretarieti imetolewa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ambapo amesema kuwa Sekretarieti ilitoa muda kwa wabunge kuwasilisha taarifa za umiliki wa mali zao na kwamba wabunge wengi hawakutekeleza agizo hilo.

“Sekretarieti iliwataka kuwasilisha nyaraka kabla ya Juni 25, 2018 zinazohusu fedha zilizoko benki au taasisi zingine za fedha, hisa, majengo, nyumba, madeni, mashine, viwanda, mitambo, magari na aina nyingine za usafiri, madeni na mikopo kwa mali zote zilizopo nje,”amesema Dkt. Tulia

Amesema kuwa mwakilishi wa Kamishna atafika ofisini kwa Katibu wa Bunge kuchukua taarifa za wabunge wote kwa ajili ya ukaguzi.

Aidha, Pamoja na taarifa hiyo Dkt. Tulia amesema kuwa kuna kundi ambalo halikuwa na taarifa kuhusu kuwasilisha vielelezo vya mali zao wataangalia jinsi ya kuwasiliana nao ili kuona vitawasilisha lini mara baada ya kurudi kwenye majimbo yao.

Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge wa Ulanga Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM) ameitaka serikali kuhakikisha uhakiki wa mali za wabunge unaenda sanjari na uhakiki wa kiwango cha elimu na taaluma zao.

 

Majaliwa atoa agizo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya
Nareel amuandalia Aika ndoa itakayoacha 'historia’