Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameagiza sekta ya fedha nchini, kuja na ubunifu utakaoiwezesha kuchangia zaidi katika pato la Taifa.

Dkt. Mpango ameyasema hayo Jijini Mwanza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali za fedha yaliyoanza Novemba 21, 2022 na yanayotarajia kufikia tamati hii leo Novemba 26, 2022.

Dkt. Philip Mpango katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha inayomalizika hii leo jijini Mwanza.

Amesema, “Nataka Wizara ya Fedha na Mipango, pande zote mbili za muungano kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, Umoja wa Mabenki Tanzania na wadau wote mfanye tafakuri kuhusu kuongeza ubunifu ili sekta hii iweze kuchangia zaidi.”

Novemba 2018 Serikali pia iliwahi kuitaka Sekta hiyo kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda na kilimo pamoja na wajasiriamali wadogo.

UNHCR yawapa tabasamu Mahabusu na Wafungwa Katavi
Nyerere na Tambo ndani ya ofisi ya ukombozi