Serikali nchini, imewekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 60 katika Sekta ya Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ili kuinua kipato cha wananchi.

Hayo yamebainishwa jijini Mwanza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah wakati wa ujio wa mabalozi nane kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya kwenye Kampasi ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA).

Mabalozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya, wakikagua shughuli za ufugaji samaki katika Kampasi ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Nyegezi jijini Mwanza.

Mwakilishi huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohammed Sheikh amesema fedha hizo zimewekezwa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kwa kununua boti na wavuvi wadogo waweze kufika kwenye maji ya kina kirefu kuvua samaki ili kuongeza kipato.

Ameongeza kuwa, ujio wa mabalozi hao ni wa kawaida ili kujionea namna utekelezaji wa miradi hiyo ambayo wanashirikiana na serikali ili kuwaondoa wavuvi katika uvuvi wa kutumia zana za zamani za uvuvi na kutumia njia ya vizimba kwa kufuga samaki wengi na kujipatia kipato zaidi.

Halmashauri zakusanya zaidi ya Bil. 485
Umoja Kenya: Viongozi wa Dini wapewa jukumu