Sakata la mchezaji kiungo wa Majimaji, Suleiman Kassim ‘Selembe’ kutoonekana kambini klabuni kwake bila taarifa sasa limechukua sura mpya.

Taarifa zilizokuwepo awali zilieleza kuwa, mchezaji huyo alikuwa akilazimisha mkataba wake uvunjwe ili aondoke, lakini sasa inaonekana kuna jambo kubwa baina yake na klabu hiyo yenye maskani yake mjini Songea mkoani Ruvuma.

Awali iliripotiwa kuwa mchezaji huyo aliondoka kambini kwa lengo la kuulazimisha uongozi wa timu hiyo kuvunja mkataba wake ili aweze kujiunga na Klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DR Congo.

Alipotafutwa Onesmo Ndunguru ambaye ndiye Msemaji wa Majimaji alisema mchezaji huyo hajaonekana klabuni na hajatoa taarifa zozote juu ya kutoonekana kwake kazini.

Alipoulizwa kuhusu sakata la kuvunja mkataba na usajili wa Motema Pembe, Ofisa huyo alisema:

Inadaiwa Selembe alizungumza na Motemba Pembe kwa ajili ya usajili, kitu ambacho ni kinyume kwa kuwa bado yupo ndani ya mkataba.

Hivyo, baada ya kuelewana na klabu hiyo ya Congo, akataka kuvunja mkataba ili akasajiliwe akiwa mchezaji huru jambo ambalo Majimaji hawakulikubali na kuamua kumgomea kuvunja mkataba.

Baada ya hali hiyo kutokea Selembe hakufurahishwa na mchakato, mwisho wake ameondoka klabuni huku akitambua ni kinyume na kanuzi za mkataba wake.

Mkemi: Yanga hatuwezi kuishangilia Simba
Kigwangalla: Najitoa kupigania maliasili zetu natukanwa na kushambuliwa