Mwanamuziki mrembo, Selena Gomez ametajwa kuwa ndiye malikia wa Instagram baada ya kuvunja rekodi ya kuwa mtu wa kwanza duniani kufikisha wafuasi (followers) milioni 100, tangu mtandao huo uanzishwe.

Selena ameweka rekodi hiyo mpya sio kwa sababu amekuwa akipost vitu vingi kwenye mtandao huo kwani tangu mwezi Agosti mwaka huu hajawahi kupost kitu chochote kwenye akaunti yake, hali inayoiongeza kiu ya mashabiki wake wanaotembelea akaunti hiyo.

Hata hivyo, Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 ameweka rekodi hiyo huku maisha ya mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari yakiwa chanzo cha kumletea ugonjwa wa msongo wa mawazo.

Hivi karibuni, Selena alitangaza kupumzika kutumia mitandao ya kijamii kutokana na kumpa msongo wa mawazo kutokana na maisha binafsi kuandamwa kwenye mitandao hiyo.

Pamoja na kufuatwa na watu milioni 100, Selena ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Justin Bieber anawafuata watu 252.

selena-insta

Selena amewafunika mastaa wengine kama Tailor Swift (Followers milioni 91.5), Beyonce (followers  milioni 85.4) na Kim Kardashian (followers milioni 83.7).

Bei ya mafuta yaanza kupanda
Video: Serikali kununua ndege 'keshi' imeepuka kuliwa - Prof. Maghembe