Kitendo cha wachezaji wa Arsenal cha kujipiga picha (Selfie) mara baada ya ushindi mnono wa mabao sita kwa sifuri dhidi ya  Ludogorets usiku wa kuamkia hii leo, kimepingwa vikali na magwiji wa soka katika ligi ya Uingereza (PL).

Richard Dunne pamoja na Rio Ferdinand wameonyesha kuwa mstari wa mbele kupinga kitendo hicho saa chache baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Emirates, kwa kusema haikupaswa kwa wachezaji hao kufanya jambo hilo.

Magwiji hao ambao waliwahi kutamba na klabu nguli za mjini Manchester (Man City na Man Utd) wamesema kitendo cha wachezaji wa Arsenal kujipiga picha (Selfie) kwa ushindi walioupata kwenye michuano ya ligi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hakionyeshi ukomavu wa kusaka mafanikio na badala yake kinadhihirisha uchanga wa akili miongoni mwao.

Wamesema bado ni mapema mno kwa wachezaji wa Arsenal kufanya jambo kama hilo, kutokana na mafanikio ya mwanzoni mwa msimu huu, kwa kuamini mambo yatawanyookea hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Ni jambo zuri kupata ushindi katika mchezo wa michuano mikubwa kama ligi ya mabingwa, lakini halina ukubwa sana kama itatokea unatwaa ubingwa katika mchezo wa fainali, hapo unaweza kuleta madoido kama ya kujipiga picha (Selfie) utakavyo,” Alisema nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya jamuhuri ya Ireland Dunne alipohojiwa na BT Sport. “Arsenal siku zote wamekua wakijisau kwa mafanikio madogo madogo kama haya na mwishowe hupoteza muelekeo na kushindwa kufanya jambo kubwa mwishoni mwa msimu.”

“Niliwahi kusema kabla, sitofanya jambo la majivuno wakati sijafikia mafanikio niliyoyakususdia mwishoni mwa msimu kama kutwaa taji,” Nilijipa matumaini haya tangu mwaka 2008 na kwa bahati nzuri tulitwaa ubingwa wa Ulaya” Wachezaji wa Arsenal wanapaswa kupevuka kiakili, wasibweteke na kujiona wameshafanikiwa kwa kuleta majivuno kwenye mitandao ya kijamii” Aliongeza Ferdinand.

Stewart Hall Arejea Kenya, Ambwaga Patrick Liewig
AS Roma Wapanga Kubomoa Ukuta Wa Man City