Polisi nchini Nigeria wamemfikisha mahakamani Seneta Dino Melaye akiwa amebebwa kwenye kitanda maalum cha wagonjwa, kujibu tuhuma zinazomkabili.

Seneta huyo amekuwa chini ya ulinzi wa polisi akiwa hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuruka kutoka kwenye gari la polisi. Hata hivyo, waliokuwa naye wanadai alisukumwa kutoka ndani ya gari.

Mahakama ya Hakimu Mkazi imeweka masharti ya dhamana kuwa $250,000 ili mtuhumiwa huyo aendelee na matibabu akiwa chini ya usimamizi wa familia na marafiki.

Seneta Melaye anatuhumiwa kugawa silaha kinyume cha sheria kwa baadhi ya watu wanaomuunga mkono kisiasa. Amekana tuhuma hizo akidai zimepikwa na watu wanaotaka kumuua kisiasa.

Seneta huyo anafahamika kwa maisha yake ya kifahari anayoyaonesha kupitia mitandao ya kijamii na hta kuimbwa na wasanii nchini humo wakiwa wanajigamba kuwa na vitu vya anasa.

Rapa Kach alikuwa msanii wa mwisho hivi karibuni kufanya wimbo alioupa jina la ‘Dino’, jina la Seneta huyo, akijigamba huku akionesha anajaribu kula dola za kimarekani na kuonesha majumba ya kifahari.

Aliyemuua mpenzi wake na kumchoma anasa mahakamani
Mabosi kampuni iliyomtapeli Majuto watupwa rumande

Comments

comments