Seneta wa Chama cha Democratic nchini Marekani, Elizabeth Warren ametoa wito wa kuanzishwa mchakato wa kuondolewa madarakani kwa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Seneta huyo wa upinzani wa jimbo la Massachusetts, ambaye ametangaza azma yake ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini humo ametoa wito huo baada ya kutolewa ripoti ya Mueller kuhusu uingiliaji wa Russia katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016.

“Kupuuza hatua ya Trump kufanya jitihada za wazi za kutaka kuzuia uchunguzi dhidi yake, kutaisababishia nchi hii matatizo makubwa na ya muda mrefu.” Amesema Elizabeth Warren Seneta wa Massachusetts.

Aidha, Bi Warren amesisitiza kuwa iwapo Rais Trump hatauzuiliwa, basi marais wajao wa Marekani watahisi kuwa wako huru kutumia vibaya mamlaka na ofisi zao.

Hivi karibuni Seneta huyo wa chama cha Democratics alisema kuwa, karibuni Trump atakuwa gerezani kabla ya uchaguzi mkuu ujao nchini humo mwaka ujao 2020, kutokana na wimbi la kashfa dhidi yake.

Hata hivyo, Mwanasiasa huyo wa Democrats amemtaja Trump kuwa matokeo ya mfumo uliochakachuliwa na anayetumikia maslahi ya matajiri walio wachache na watu wenye ushawishi, huku akiwapaka matope wapinzani na wakosoaji wake.

Video: Serikali yataka kila mtanzania kumiliki laini moja ya simu
Video: Hakuna Alikiba bila Diamond wala Diamond bila Alikiba, tazama ngoma zao hapa chini