Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli Julai 2, 2018 amezindua kitabu cha Dkt. Reginald Abraham Mengi kilichopewa jina la ‘I Can, I Must, I Will- The Spirit of Success’ katika hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amezungumza mambo mabli mbali ambapo moja ya mambo hayo ni namna gani watanzania wanapaswa kujifunza na kuacha kukatishwa tamaa katika safari za mafanikio yao. Hapa kuna Sentensi 5 ambao Rais Magufuli amezungumza;

“Kitabu cha Mzee Mengi kiwe fundisho kwetu sote, nitoe wito kwa wafanyabiashara wote msisikilize maneno ya watu wanao wakatisha tamaa, fanyeni biashara kweli kweli” – Rais Dkt. Magufuli.

“Watanzania tuache kukatishana tamaa na ninafahamu katika historia ya Mzee Mengi yapo mengi amepambana nayo ya kukatishwa tamaa” – Rais Dkt. Magufuli

“Nilisoma kwamba aligongwa na gari siku ya mahafari yake, lakini hajakata tamaa hana uwezo wa kuandika kupitia mikono yake, lakini anaweza kuandika anachokifikiria kwa kutumia ulimi wake, nitamchangia Sh10 milioni iweze kumsaidia katika mawazo yake anayoyapata kutoka kwa Mwenyezi Mungu,” – Rais Magufuli.

“Nilijua ukishakuwa Rais huwezi kukatishwa tamaa na mtu yeyote kwa sababu wewe ni Rais lakini haikuwa hivyo, nilipoingia niliyaona” – Rais Magufuli

“Nina matumaini makubwa kupitia kitabu chako hiki watanzania wengi watajenga matumaini, kujiamini na mafanikio makubwa na katika hili naomba kitabu hiki ukitafasiri kwa lugha ya kiswahili ili kupata fursa ya watanzania wengi kukisoma” -Rais Dkt. Magufuli

“Funzo la kwanza nililolipata kutoka kwenye kitabu hichi alichokiandika Mzee Mengi kuwa sisi Watanzania tukiamua tutafanikiwa” – Rais Magufuli.

Daktari bingwa afunguka kuhusu magonjwa ya Moyo
Mengi atoboa siri ya kutunga kitabu chake

Comments

comments