Mshauri Mkuu ndani ya Klabu ya Young Africans kwenye mchakato wa kuelekea mabadiliko Senzo Mazingiza Mbatha, amesema anatambua michuano ya Kombe la Mapinduzi ni kama ‘BONANZA’ lakini utambuzi huo hautoshi kusitisha furaha ya kuwa mabingwa kwa mwaka huu 2021.

Senzo ambaye aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba SC kabla ya kutimkia Young Africans mwezi August 2020, amesema furaha kubwa waliyonayo ni kuwafunga mabingwa wa Tanzania Bara kwenye michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka tangu 2007, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

“Najua michuano ya Kombe la Mapinduzi ni kama “BONANZA’ lakini jambo kubwa tumekua mabingwa na nzuri zaidi tumewafunga mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC.”

“Haijalishi ukubwa ama udogo wa michuano, lakini unapokutana na timu imara kama Simba SC unapaswa kuwa imara zaidi, na ndicho walichokifanya wachezaji wetu na leo (Jana) wanashangilia mafanikio yao.” Amesema Senzo ambaye alikua sehemu ya mashuhuda wa mchezo wa fainali mjini Unguja-Zanzibar.

Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2021 ilifikia tamati jana usiku, kwa kikosi cha Young kuibuka mabingwa kwa kuwabanjua Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kwa changamoto ya mikwaju ya penati nne kwa tatu.

Timu zilizoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu 2021 kutoka Zanzibar ni Jamhuri, Chipukizi, Malindi FC na Mlandege, huku Young Africans, Simba SC, Namungo FC na Azam FC zikitokea Tanzania Bara.

Onyango ampigia 'SALUTI' kocha Matola
Taifa Stars ya 'CHAN' yakabidhiwa mzigo