Kufuatia kikao kilichofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau pamoja na wamiliki wa televisheni nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wamekubaliana kuanzia septemba 5 mwaka huu visimbusi vitaanza kuonesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Serikali imefikia uamuzi huo baada ya visimbusi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana na aina ya leseni zao.

”Kuanzia septemba 5 mwaka huu, visimbuzi vya Ting, Starmedia, Continental na Digtek vitaonesha takribani channeli  34 za ndani bure, ili kutoa fursa ya kila mwananchi kuwa na  haki ya kupata taarifa” alisema Dkt. Abbasi

Aidha, alielezea kuwa wadau hao na wamiliki wa televisheni wameonesha kuridhishwa na hatua hiyo kwa vile Serikali imetengeneza miundombinu itayoruhusu channeli zao kuonekana nchi nzima.

Dkt. Abbasi, alisisitiza kuwa “nchi imeandaa mfumo, ambao unaweza kufanya kazi bila kutegemea kampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha channeli za ndani au matangazo, kwa hivyo wadau au wamiliki wa vyombo vya habari wasihofu kuhusu hilo”

Kikao kati ya Waziri Mwakyembe na wadau  na wamiliki wa televisheni  nchini, kimefanyika kwa lengo la kufanya majadiliano ya pamoja baina serikali na wadau hao ili kupata muafaka kuhusu kutooneshwa kwa chaneli za ndani katika visimbusi vilivyokiuka masharti ya leseni zao.

Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, pamoja na wataalamu wake.

 

Video: Msimamo wa Dk Mpango dhidi ya Makonda mjadala, Mtikisiko Bungeni
Kevin Strootman kukipiga Ufaransa