Mwanadada kutoka nchini Marekani Serena Williams, amefaulu kuingia katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Wimbledon, baada ya kutumia mbinu mbadala na kumshinda mpinzani wake kutoka Urusi, Svetlana Kuznetsova.

Serena alionyesha kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Kuznetsova, katika seti ya kwanza lakini alijitahidi na kurejea mchezoni.

Mpaka mpambano huo unamalizika, Serena aliibuka na ushindi wa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 7-5 na 6-0.

Katika seti ya kwanza Russian Kuznetsova anayeshika namba 13 kwa ubora duniani upande wa kina dada, alitangulia kwa kuonyesha dhamira ya kumshinda Serena kwa 5-4, lakini mambo yalimgeukia na kujikuta akipoteza seti hiyo kwa 7-5.

Michezo mingine ya hatua ya mzunguuko wa wa nne kwa wanawake ilishuhudia;

Simona Halep [5] akimshinda Madison Keys [9], seti mbili kwa moja ambazo ni 6–7, 6–4 na 6–3.

Venus Williams [8] akimshinda Carla Suárez Navarro [12], seti mbili kwa sifuri ambazo ni 7–6 na 6–4

Angelique Kerber [4] akimshinda Misaki Doi, seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6–3 na 6–1

Dominika Cibulková [19] akimshinda Agnieszka Radwańska [3], seti mbili kwa moja ambazo ni 6–3, 5–7 na 9–7.

Elena Vesnina akimshinda Ekaterina Makarova, Seti mbili kwa moja ambazo ni 5–7, 6–1 na 9–7.

Michezo ya hatua ya robo fainali kwa wanawake ambayo itachezwa kuanzia leo;

Romania Simona Halep [5] kutoka nchini romani atapambana na Angelique Kerber [4] wa Ujerumani.

Serena Williams [1] kutoka nchini Marekani atapambana na Anastasia Pavlyuchenkova [21] wa Urusi.

Venus Williams [8] kutoka nchini Marekani atapambana na Yaroslava Shvedova wa Kazakhstan.

Dominika Cibulková [19] kutoka nchini Slovakia atapambana na Elena Vesnina wa Urusi.

Muhimu: kwenye mabano ni nafasi ya ubora kwa mchezaji kwa mujibu wa viwango vya dunia.

Ugonjwa Usiojulikana Umeendelea Kuenea Dodoma na Manyara
Video Mpya: Harmonize - Matatizo