Mwanadada kutoka nchini Marekani, Serena Williams ameendelea kujiweka katika daraja tofauti na wachezaji wengine wa kike kwenye mchezo wa tennis duniani, baada ya kufanikiwa kumshinda mpinznai wake kutoka nchini Poland, Agnieszka Radwanska katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya Australian Open.

Serena, amejiweka katika ramani tofauti duniani, kutokana na kutinga katika fainali ya saba ya michuano ya Australian Open, rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na mshiriki mwingine yoyote upande wa wanawake.

Katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliochezwa mapema hii leo, Serana alifanikiwa kumshinda Radwanska, kwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6-0 na 6-4.

Hatua hiyo, inaendelea kumpa nafasi mwanadada huyo wa kimarekani, kukaa kileleni mwa msimamo wa viwango vya ubora duniani upande wa wanawake na tayari kuna baadhi ya mashabiki wake wanaamini atafanikiwa kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.

 Angelique Kerber (Kulia) Akimpa pole Johanna Konta baada ya kumshinda katika mchezo wa nusu fainali.

Katika hatua ya fainali, Serana atapambana na Angelique Kerber kutoka nchini Ujerumani, ambaye alifanikiwa kumshinda mpinzani wake Johanna Konta wa Uingeereza katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Rais Magufuli amteua naibu Gavana wa benki kuu
Novak Djokovic Ni Zaidi Ya Roger Federer