Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo Mei 21, 2017 inarusha karata muhimu katika mchezo dhidi ya Niger katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON U-17.

Serengeti Boys itaingia Uwanja wa Port Gentil huku mkononi ikiwa na pointi 4 ilizovuna katika michezo yake miwili ya awali kwani ilianza kupata sare tasa dhidi ya Mali Mei 15, mwaka huu kabla ya kuifunga Angola Mabao 2-1 katika mechi zilizofanyika Uwanja wa l’Amitee jijini Libreville.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime amesema kuwa mchezo huo ni mhimu kwani vijana wako vizuri na wana ari ya mchezo

Trump kutoa hotuba yake falme za kiarabu
Korea ya Kaskazini yafanya jaribio lingine