Shirikisho la Soka nchini TFF limetoa orodha ya wachezaji 22 wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ watakaosafairi kuelekea Morocco kwa ajili ya fainali za Afrika z vijana (AFCON U17).

Tanzania itawakilishwa na Serengeti Boys kwenye fainali hizo zitakazoanza Machi 13 hadi 31 katika viwanja vya El Bachir, Moulay Hassan na Père Jégo.

Tanzania imepangwa Kundi B na itaanza kusaka ubingwa wa fainali hizo kwa kucheza dhidi ya Nigeria Machi 14, mchezo wa pili itacheza dhidi ya Algeria Machi 17 na itamaliza hatua ya makundi kwa kupapatuana na Congo Brazzaville Machi 20.

Michezo miwili dhidi ya Nigeria na Algeria, Tanzania itacheza kwenye uwanja wa El Bachir kabla ya kumalizia kwenye uwanja wa Moulay Hassan itakapocheza dhidi ya Congo Brazzaville.

Kundi A katika fainali hizo kuna timu za mataifa ya Morocco, Uganda, Zambia na Ivory Coast huku Kundi C lina timu za mataifa ya Cameroon, Senegal, Mali na Afrika Kusini.  

Timu nne zitakazotinga hatua ya nusu fainali zitafuzu moja kwa moja kucheza fainali za Kombe la Dunia chini ya umri wa miaka 17, zitakazofanyika nchini Peru baadae mwaka huu.

Orodha ya kikosi cha Tanzania ‘Serengeti Boys’ kinachoondoka kuelekea Morocco.

May be an image of text that says ".TFF. Û) KIKOSI CHA WACHEZAJI 22 CHA U-17 SERENGETI BOYS KINACHOSAFIRI KWENDA MOROCCO KWENYE FAINALI ZA AFCON 2021 Shomari Mbwana Mnyamani Said Naushad Said Liptone Eliabi Mlagulwa Abdulkarim Kassim Kiswanya Abubakar Abudallah Sabian Omary Hassan Yahya Abdurahman Juma Khery Mohamed Saad Hussein Kelvin Joel Komba Omar Abbas Mvungi Omary Bakari Omary Abdallah Hamisi Hassan Sylvester Sylvester Otto Ahmed Khalid Chambera Baraka Sylvester Nyamkindo Kassim Ibrahim Yahya Ismail Mpank Bombama Hijjah Shamte Lidah Ladaki Juma Chasambi Kamli Jesto Masanja Abdulah Mussa Libandika Abubakari Ramadhani Lubotile KOCHA MKUU: HABABUU ALI TanFootball TFFTanzania TFF TV Play fair, Be Positive"
Kesi ya mauaji ya Khashoggi yaanza tena
Kocha Mgunda aichimba mkwara Young Africans