Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imelazimisha sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Afrika Kusini Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Magharibi mwa Mji wa Johannesburg.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za U-17 Madagascar mwakani, mabao yote yalipatikana kwa penalti kipindi cha pili.

Afrika Kusini walitangulia kwa bao la Luka de Roux dakika ya 65, kabla ya Ali Mtengi kuisawazishia Tanzania dakika ya 75.

Sasa Serengeti itahitaji hata srae ya 0-0 katika mchezo wa marudiano Agosti 21, Uwanja wa Azam Compolex, Chamazi, Dar es Salaam ili kusonga mbele hatua ya mwisho ya mchujo.

Jipu Lanukia Dawasco
Mtibwa Sugar Waibana Young Africans