Timu ya taifa ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo asubuhi imeondoka jijini Dar es Salaam, kwenda mjini Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya kambi ya siku 10 kabla ya kuivaa Congo-Brazzaville katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania nafasi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.

Serengeti Boys imejipanga kuitumia kambi hiyo kama sehemu ya kumaliza mtihani unaowakabili dhidi ya Congo Brazzaville ili kufanikisha azma ya kutinga kwenye fainali za afrika kwa vijana za mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Masdagascar.

Kocha mkuu wa Serengeti Boys Bakari Shime, amewatoa shaka baadhi ya mashabiki wa soka walioonyesha kukata tamaa kuelekea mchezo wao wa Oktoba 2 utakaochezwa mjini Brazzaville.

Shime amesema watanzania wote kwa pamoja bado wanatakia kuiamini timu yao kutokana na kuwa na mikakati mziuri ya kwenda ugenini na kupata ushindi kama ilivyokua kwenye michezo iliyotangulia.

Amesema yeye kama kocha hana shaka yoyote kutokana na kuamini hakuna litakaloshindikana katika mchezo wa mkondo wa pili, hasa ikizingatiwa tayari kuna baadhi ya madhaifu ya timu pinzani ameshayasoma na kuyatafutia ufumbuzi.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita, Serengeti Boys ilishinda mabao 3-2, na endapo itahitaji kusonga mbele itatakiwa kusaka matokeo ya sare ama ushindi kwenye mchezo wa Oktoba 2.

Asilimia 80 ya walimu shule za msingi Uganda hawajui kusoma
Ryan Giggs Kumrithi Francesco Guidolin?

Comments

comments