Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imefanikiwa kushinda ubingwa wa michuano ya vijana wa mataifa ya kusini mwa Afrika COSAFA nchini Botswana.

Katika mchezo wa fainali ambao Serengeti Boys imepambana na Angola, ulimalizika kwa vijana hao kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Bao la kwanza ni la vijana wa Angola, ambalo lilipatikana katika dakika ya 38 kupitia kwa Morais huku bao la kusawazisha la Serengeti Boys likipachikwa katika dakika ya 74 kupitia kwa Pius.

Ikumbukwe Serengeti Boys imeshiriki michuano hiyo kama mwalikwa ambapo imeweza kutumia nafasi iliyopata na kushinda ubingwa huo kwa mara ya kwanza.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 hapo mwakani, ambapo kikosi hicho cha Serengeti Boys ndicho kitakacholiwakilisha taifa.

Video: Magufuli akata mzizi wa fitna, SSRA yafafanua zaidi mafao ya uzeeni, Vigogo watumbuliwa kukatika umeme
RC Wangabo atoa tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kwa waathirika wa mvua kali Rukwa