Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, iliwasili uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, usiku wa October 4, 2016 ikitokea Congo

Baada ya mechi dhidi ya Congo Brazzaville na kufungwa goli moja katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa mataifa ya Afrika  kwa wenye umri chini ya miaka 17 ambayo yatafanyika 2017 Madagascar.

Vijana hao ambao wametolewa kwa kufungwa magoli mengi nyumbani, walienda Congo wakiwa na ushindi wa goli  3-2, hivyo kufungwa goli 1-0 kunawafanya watolewe kwa kigezo cha kuruhusu kufungwa magoli mengi nyumbani licha ya kuwa aggregate inayosomeka 3-3.

ZFA Yawakaribisha Young Africans Uwanja Wa Amaan
Msajili wa vyama vya siasa awageukia wadau wa habari na kutoa onyo kali