Beki wa kulia wa klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) Serge Aurier, ameshindwa kusafiri na kikosi cha klabu hiyo ambacho kipo jijini London, tayari kwa mpambano wa mzunguuko wa tano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Arsenal.

Hukumu ya kesi ya kumpiga kiwiko askari polisi iliyoamuru apelekwe jela kwa miezi miwili, imekua chanzo cha beki huyo kutoka nchini Ivory Coast kuzuiwa kuingia jijini London.

Hata hivyo Aurier alipinga adhabu ya kufungwa jela iliyotolewa dhidi yake mwezi Septemba kwa kukata rufaa, na bado taratibu za kisheria zinaendelea kuunguruma mahakamani .

Taarifa zilizothibitishwa na uongozi wa klabu ya PSG zinaeleza kuwa, Aurier hatokua sehemu ya kikosi cha klabu hiyo katika mchezo wa leso usiku, na wamejiandaa kikamilifu kuliziba pengo lake.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo umetanabaisha kuwa, mara kadhaa wamekua wakijitahidi kulimaliza suala la Aurier ili aweze kuwa huru kwa ajili ya kucheza soka, lakini bado mambo yamekua tofauti.

Arsenal watapambana na PSG hii leo huku ikiwa imeshafuzu kucheza mzunguuko wa 16 bora kwa kufikisha point 10, sambamba na wapinzani wao kutoka nchini Ufaransa.

Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao moja kwa moja, na Aurier alikuwa sehemu ya kikosi cha PSG.

Mzimu Wa Majeraha Wamuandama Vincent Kompany
Bruce Arena Abebeshwa Mzigo Marekani