Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero, atakosa mchezo muhimu wa ligi kuu ya soka nchini England utakaochezwa baadae dhidi ya Tottenham Hotspur.

Manchester City wanahitaji point tatu ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa msimu huu, bada ya kushindwa kufanya hivyo mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Manchester United katika uwanja wao wa Etihad.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, alishindwa kuendelea mazoezi siku mbili zilizopita, baada ya kuumia goti.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amesema Aguero alishindwa kufanya mazoezi baada ya kupata maumivu hayo, dakika za awali.

“Aguero ameumia, hatocheza  dhidi ya Spurs,” alisema Guardiola katika mkutano wa waandishi wa habari.

Guardiola amethibitisha kuendelea kukosa huduma ya mabeki  John Stones na Benjamin Mendy ambao ni majeruhi wakati kiungo Fernandinho akitumikia adhabu ya kadi.

Manchester City imepoteza michezo mitatu mfululizo ndani ya majuma mawili kwa mara ya kwanza chini ya Guardiola.

Kocha Mayanga atajwa kurithi mikoba nchini Kenya
Young Africans kuifuata Wolaita Dicha kesho jumapili

Comments

comments