Wakala wa mshambuliaji kutoka nchini Colombia na klabu ya AC Milan Carlos Bacca, amesema anaamini mchezaji huyo atabaki San Siro.

Bacca amekua katika minong’ono ya kuwa mbioni kuihama AC Milan, itakapofika mwezi Januari mwaka 2017, na klabu yake ya zamani ya Sevilla inapewa nafasi kubwa ya kumsajili.

Wakala wa mshambuliaji huyo Sergio Barila ameiambia tovuti ya habari za michezo iitwayo Tuttomercatoweb: “Kwa nini aondoke? Matatizo kati ya mtu na matu hayawezi kuwa sababu ya kumshurutisha kuondoka, naamini ataendelea kucheza San Siro.

“Usajili wa dirisha dogo? Hainiingii akilini. Kutakiwa na klabu ya Valencia? Kwa kweli sijui chochote kuhusu mambo hayo. Alihoji na kujijibu mwenyewe.

“Carlos anataka kubaki AC Milan, na Milan wanapendezwa na uwepo wake. Amedhamiria kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na The Rossoneri.

Bacca anahusishwa na taarifa za kutokua na maelewano na meneja wa Ac Milan Vincenzo Montella

Ndege iliyobeba wachezaji soka wa Brazil yaanguka, watu 76 wafariki dunia
Gareth Southgate Kusaini Mkataba Wa Miaka Mitatu