Kipa wa Manchester United Sergio Romero amesaini mkataba mpya utakaomfanya abaki katika klabu hiyo mpaka ifikapo mwaka 2021.

Romero mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Manchester United mwaka 2015 akitokea katika klabu ya Sampdoria ya nchini Italy.

”Nani asingependa kuwa katika klabu kubwa duniani, nimefurahi kusaini mkataba mpya” alisema Romero. Kipa huyo aliongeza kuwa alijiskia furaha kuwa katika kikosi kilicho shinda kombe la Europa Legue na anataka kuisaidia timu yake kufanya vizuri msimu ujao.

 

Mlinda mlango huyo ambaye ni namba moja katika timu ya taifa ya Argentina amecheza katika kikosi cha kwanza cha Man Utd mara 28, mara sita tu katika hizo ikiwa ni katika michezo ya ligi kuu ya Uingereza.

Mkataba wa Romero umekuja  wakati ambapo Real Madrid wamerudi katika mbio za kutaka kumsajili goli kipa namba moja wa Man Utd David De Gea.

 

 

Associazione Calcio Milan Yakamilisha Kwa Lucas Biglia
Nolito Arudi Nyumbani Hispania

Comments

comments