Katibu Mkuu wa (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa Watanzania hawana shauku wala ndoto ya kufanya mabadiliko ya utawala kwa kuwategemea wanasiasa wenye mtazamo na mawazo duni.

Ameyasema hayo katika kipindi ambacho Serikali ya CCM ikijibadili mfumo na kisera kukidhi matakwa ya wananchi na wakati vyama vya siasa vya upinzani vikitarajia kushika dola.

Shaka ametoa kauli hiyo wakati aliposhiriki mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya Morogoro Open School

“Tofauti ya kati ya viongozi CCM na wa vyama vingine, viongozi wa Serikali ya CCM hujikuta katika kujadili hoja na utekelezaji wa mipango na si kuishi kwa nadharia isiyo na tija. Serikali ya CCM itabaki kuamini katika siasa ya ujamaa na kujitegemea. Tangu zama za sera za uchumi hodhi na ujio wa soko huria na utandawazi, CCM imekataa kushikilia ukale bali hufanya mabadiliko ya kisera,”amesema Shaka

Aidha, amesema kuwa anayefikiria siasa ya ujamaa na kujitegemea imekufa hawana uelewa kwani serikali inaposomesha wanafunzi bure, kutoa huduma bora za afya ni katika utekelezaji wa msingi ya ujamaa.

Katibu huyo wa CCM amesema wanasiasa hawapaswi kukosoa kwa pupa na jazba badala yake bali wawe na vipimo vya uhalisia wa madai yao kwani wananchi ni werevu, wanajua kutofautisha yaliyokuwepo na ufanisi wa mabadiliko yanayooneka.

Shaka amehimiza wanafunzi kuendelea kujenga matumaini kwa sera za CCM kwani ndicho chama chenye uwezo wa kufanyakazi kwa uhodari katika kuleta maendeleo.

“Nawawatia shime wanafunzi mjipe jukumu la kusoma kwa bidii. Wale waliohitimu watambue wana jukumu la kujiandaa mwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali pia mshiriki ushindanikwenye soko la ajira” amesema Shaka

Watanzania msitegemee kupata kirahisi kitambulisho cha taifa- Kangi Lugola
Kiama cha Mawaziri, wabunge watoro bungeni chaja