Serikali imesema kuwa hakuna maiti ambayo inashikiliwa kwenye Hospitali yoyote nchini kwasababu ya madai ya fedha za matibabu kwani kila hospitali ina Dawati la Ustawi wa Jamii ambalo hushughulikia suala hilo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu maswali ya wabunge ambao waliitaka Serikali kuacha tabia ya kushikilia miili ya wanaofariki na ndugu zao kushindwa kulipa gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaofariki badala yake iwasamehe.

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mussa Mbarouk wa Tanga waliibua hoja hiyo wakati wakichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Sugu alisema Serikali imekuwa ikisema hakuna Mtanzania anayekosa matibabu lakini wanashikilia maiti hospitalini na hatua hii inawanyima Watanzania kwenda kufanya ibada kwa ndugu zao wanaofariki kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amejibu hoja hiyo kwa kusema Wananchi wanaokosa fedha za kulipia matitabu wanapaswa kwenda kwenye Dawati la Ustawi wa Jamii linalokuwepo katika kila Hospitali na hakuna maiti ambayo inashikiliwa.

Hamann amkataa Leroy Sane, ampigia chepuo Milot Rashica
Tetesi za usajili: Wanaotajwa kuzihama klabu zao mwishoni mwa msimu wa 2019/20