Wananchi waliokumbwa na zoezi la bomoabomoa katika maeneo ya mabondeni wametakiwa kutotarajia kupewa viwanja na serikali kwani viwanja hivyo havipo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki aliyasema hayo jana jijini humo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema kuwa serikali haina viwanja vya kuwatosha familia zaidi ya 8,000 zilizokumbwa na zoezi la bomoabomoa waliokuwa wanaishi kinyume cha sheria katika maeneo ya mabondeni ikiwemo bonde maarufu la Msimbazi.

“Serikali haina viwanja vya kutosha vya kuwagawia zaidi ya familia 8,000 zitakazobomolewa, niwashauri tu wasiendelee kupoteza muda wao kwa kuwasikiliza wanasiasa, watafute makazi mengine waende. Kama walivyovamia na kujenga ndivyo wanavyotakiwa kutafuta maeneo mengine wahamie,” alisema mkuu huyo wa mkoa.

Akitoa ufafanuzi kuhusu viwanja vinavyotolewa kwa wananchi katika eneo la Mwabwepande, alisema jumla ya viwanja 1,007 vilitolewa kwaajili ya watu walioathirika na mafuriko mwaka 2011 ambao waliwekwa katika kambi maalum, na sio kwa ajili ya wananchi wanaobomolewa hivi sasa.

 

Koke Aitabiria Mambo Mema Atletico Madrid
Waliovamia shamba la Sumaye watimuliwa