Serikali imepanga kuwasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii yatakayoanzisha Fao la Upotevu wa Ajira kwa wafanyakazi watakaokuwa wanapoteza ajira kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kazi.
Hayo yamesema hii leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, ambapo amesema kuwa Serikali inatambua changamoto ya wingi wa mifuko inayoikabili Sekta ya Hifadhi ya Jamii hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo mwaka 2015 Serikali ilifanya tathamini ya mifuko yote ya Pensheni kwa lengo la kuangalia uwezekano na namna bora ya kuiunganisha.
“Matokeo ya tathimini iliyofanyika mwaka 2015 yalionyesha kuwa inawezekana kuunganisha mifuko hiyo na kubaki na michache kwa kuzingatia hali halisi ya mahitaji,”amesema Mavunde.
Aidha, Mavunde meongeza kuwa Serikali imeandaa mapendekezo ya kuunganisha Mifuko mitano inayotoa mafao ya pensheni na kubaki na michache iliyo imara ili kuweza kuondokana na usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza.
Hata hivyo, amesema kuwa Kwa mujibu wa Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa mwaka 1952 fao la kujitoa sio miongoni mwa mafao yalioainishwa katika mkataba huo.

Video: Tumemchoka Mange - DCI, Magufuli awaonya viongozi wastaafu
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 12, 2017