Serikali imepanga kuanzishwa vituo vitakavyofanya kazi ya kuhakiki ubora wa bidhaa za wafanyabiashara kabla ya kupeleka nje ya nchi ili kujua kama vina ubora wa Kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa biashara kutoka sekta mbalimbali nchini ulioandaliwa na Mradi wa kuwasaidia Wakulima kuongeza thamani ya mazao na namna ya kufikia Masoko (MARKUP), amesema kukosekana kwa vituo vya kuhakiki bidhaa nchini imekuwa ikichangia kurudisha nyuma uendeshaji wa biashara hizo kwa wafanyabiashara nchini.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara wanapata wakati mgumu katika kuhakiki mpaka kupeleka kwanza nje kuhakikiwa ndipo kuziingiza tena sokoni, ambapo leo Machi 11 Chama cha kuhakiki ubora huo wa bidhaa za kwenda nje ya nchi na kabla ya kuingia nchini kinazinduliwa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi huo wa MARKUP, Safari Fungo amesema katika tafiti walizofanya, wamebaini changamoto mbalimbali ambazo wafanyabiashara wanakutana nazo katika uingizaji na upelekaji wa bidhaa nje ya nchi.

Katika utafiti huo asilimia 50 ya changamoto zilizopo kwenye biashara zipo kwa wafanyabiashara kushindwa kukidhi mahitaji ya soko ya ubora na viwango kwenye masoko ya nje .

Waziri Mkuu wa Ivory Coast afariki dunia
Zambia waomba uenyeji AFCON U17