Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imenza rasmi mchakato wa kumnyang’anya shamba Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kwa kulimiliki muda mrefu bila kuliendeleza.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri mwenye dhamana, William Lukuvi alisema kuwa tayari wameshampa notisi kisheria na kinachosubiriwa ni sahihi ya Rais John Magufuli kuhalalisha uamuzi huo.

”Kama wewe ulifikiri kwa sababu ni Waziri Mkuu hatutachukua hatua, sasa umejibiwa kwamba tumechukua na Ofisa aliyechukua hatua yule pale,” alisema Waziri Lukuvi. ”Sisi katika utendaji wetu hatuangalii sura ya mtu,” aliongeza.

Shamba hilo linaloingia mikononi mwa Serikali, ni lile liliko katika eneo la Mwabwepande jijini Dar es Salaam ambalo mwishoni mwaka jana, wananchi waliobomolewa nyumba zao walilivamia na kujenga.

Aidha, Waziri Lukuvi aliwataka wananchi kutojichukulia hatua ya kuvamia maeneo yaliyokaa muda mrefu bila kuendelezwa badala yake watoe taarifa wizarani ili hatua za kisheiria zifuatwe.

Alisema kwa kawaida notisi hiyo hutolewa kwa mhusika na baada ya siku 90 hupelekwa wizarani kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Rais ambaye atachukua uamuzi kwa kushauriwa na wizara hiyo.

Sumaye aliwahi kueleza kuwa ameliacha eneo kwani lengo lake ni kujenga chuo kikuu na sio vinginevyo. Aliweka wazi nia yake ya kufika mahakamani endapo atanyang’anywa eneo hilo.

David Moyes Kujibu Mashtaka, Hasira Zamponza
Shule ya Sekondari Almuntazir ya jijini Dar yapigwa faini mil. 25 kwa uchafuzi wa mazingira