Serikali imeingiza nchini jumla ya tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia pamoja na tani elfu 23 za mbolea ya kupandia kupitia mfumo mpya wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja, lengo likiwa ni kudhibiti bei kwa kuzingatia bei elekezi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA), Lazaro Kitandu alipokuwa akizungumza na waandishi habari hii leo ambapo amesema kuwa mpaka sasa jumla ya tani elfu 55 za mbolea zimewasili nchini.

Amesema kuwa awamu hii ni ya kwanza ya kuingiza mbolea nchini kupitia mfumo mpya ya uagizaji mbolea kwa pamoja ambapo kampuni ya OCP S.A ya nchini Morocco imeingiza jumla ya tani elfu 23 za mbolea ya kupandia na Kampuni ya Premium Agro Chem imeingiza tani elfu 32 za mbolea ya kukuzia.

“Mpaka sasa zoezi la kupakua mbolea ya kupandia (DAP) tani elfu 23 linaendelea vizuri na mara baada ya kumaliza kupakua mbolea hii tutaanza zoezi la kupakua mbolea ya kukuzia (UREA) ambayo ni tani elfu 32,” amesema Kitandu.  

Hata hivyo, Kitandu ameongeza kuwa Waziri wa kilimo amesisitiza kusimamiwa kwa bei kila ngazi kwasababu taasisi peke yake haiwezi kuwa na watu kila mahali hivyo Tawala za mikoa, Serikali za mitaa mpaka Kijiji zitasaidia kusimamia bei ambazo zimetolewa.

 

Video: Majaliwa aguswa na Masenga, ampa msaada wa milioni 10
Lowassa amtembelea Lissu hospitalini Nairobi, aeleza alichokiona