Kaimu Kamishna Msaidizi (Uchumi na Biashara ya Madini), Godleader Shoo amesema kuwa Wizara ya Madini itafanya mnada kwa mara ya kwanza wa madini ya Tanzanite kutoka kwa kampuni nne za uchimbaji wa madini hayo zilizopo Mererani wilayani Simanjiro.

Amesema kuwa mnada huo utafanyika Oktoba 15, mwaka huu ambapo utaratibu wa kufanya mnada huo ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje ya nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei ya ushindani inayoendana na soko la dunia.

Aidha, amezitaja kampuni zitakazouza madini katika mnada huo kuwa ni TanzaniteOne, Franone, Glitter Germs na Classic Gems. na kuongeza kuwa zitauza madini ghafi na yaliyokatwa.

“Mnada huu utaendeshwa kwa usalama mkubwa kwa kuwa madini ya Tanzanite yana thamani kubwa. Serikali imeimarisha ulinzi ili kujihadhari na watu wasio waaminifu,” amesema Shoo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa minada kama hiyo pia hufanyika kwa nchi za Afrika zenye madini ya vito kama vile Zambia (emerald), Zimbabwe (almasi) na Afrika Kusini (almasi).

Mahakama yaamua ya aliyekamatwa kwa kudai Mugabe ni ‘Mzee…’
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 13, 2017

Comments

comments