Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuzingatia maelekezo Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na maeneo yote yaliayoainishwa katika ilani ya chama hicho pamoja na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo hii leo Desemba 8, 2022 wakati akizungumza katika Mkutano mkuu wa 10 wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mpinduzi Taifa, jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya serikali ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika miradi ya maendeleo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, Serikali itaendelea kufanyia kazi maeneo yote yenye changamoto na kuhakikisha inasimamia miradi yote ya kimaendeleo kwa uadilifu na kuongeza kuwa ilani ya CMM ni lazima isimamiwe ili kuleta ufanisi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kupokea maelekezo mbalimbali ili kuimarisha utendaji kazi weny wenye uadilifu na uaminifu.

Wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji Tabora
Bima yawalipa Marubani waliofariki ajali ya ndege Bukoba