Serikali kupitia Wakala wa Serikali Mtandao (Ega) imepanga kuthibiti matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wake wakati wa muda wa kazi ili kuongeza ufanisi katika ofisi za umma.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao (Ega), Suzan Mshakangoto amesema kuwa Serikali imelenga zaidi mitandao ya Whatsap, Facebook, Instagram na Twitter kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.

Mshakangoto alieleza kuwa tayari sehemu kubwa ya wataalamu wa Tehama wa Serikali wameshapewa mafunzo kuhusu namna ya kudhibiti matumizi ya mitandao hiyo ili kuongeza ufanisi kwa watumishi wakati wa mida ya kazi.

Hatua hii inachukuliwa na Serikali ikiwa ni miezi michache tangu aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuitaka Ega kuangalia namna ya kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii katika ofisi za serikali.

Hata hivyo, utekelezaji huo unaweza kuchukua muda kwani hadi sasa ni taasisi 72 pekee za Serikali ambazo zimeunganishwa kwenye mkongo wa Taifa kati ya taasisi zaidi ya 500.

 

Louis Van Gaal Awafikishia Ujumbe Zomea Zomea
Simba Kuboresha Benchi La Ufundi