Serikali imetoa boti yenye thamani ya zaidi ya shilingi billion nne ili kusaidia doria katika mwambao wa bahari mkoani Tanga lengo likiwa ni kukabiliana na uingizwaji wa bidhaa zinazopitishwa kwa njia ya magendo ili kukwepa kodi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela ambapo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa boti hiyo inafanya kazi kwa saa 24.

Amesema kuwa kwa sasa wafanyabiashara wa magendo wasifikiri tena kuna njia katika pwani ya bahari ya Hindi hivyo ameagiza meli hiyo ifanye kazi ipasavyo.

Hata hivyo, kwa upande wake meneja wa bandari mkoa wa Tanga, Percival Salama amesema uboreshaji wa Bandari hiyo unaoendelea ambapo mpaka sasa ujenzi wa gati namba mbili unaoendelea bandarini hapo umefikia karibu asilimia 70 wa wanatarajia ifikapo mwezi wa sita itakua imekalika.

DC Kassinge aitaka Seminari ya Kidugala kumalizana na Mkurugenzi
Makonda atuma ujumbe kwa Lowassa, Msigwa na ... 'tusijaribiane'