Serikali kupitia Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma imesema itaendelea kushirikisha jamii, faida za Bima ya Afya kwa Wote pamoja na afua mbalimbali za afya.

Hayo yamebainishwa mkoani Morogoro na Mratibu wa Mawasiliano ya afya na mabadiliko ya tabia katika jamii, Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya, Peter Mabwe wakati akifunga kikao cha kamati ya kitaalam ya ushauri wa Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii (CBHP-TAC).

Mratibu wa Mawasiliano ya afya na mabadiliko ya tabia katika jamii ,Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Peter Mabwe akifunga kikao cha kamati ya kitaalam  ya ushauri wa  Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii (CBHP-TAC).

Kkatika kikao hicho, chenye lengo la uimarishaji afua za huduma za afya ngazi ya jamii kilichoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo PACT -Tanzania na BMF, Mabwe amesema ushirikishwaji katika uboreshaji wa huduma ngazi ya jamii ikiwemo umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote ni muhimu katika kuimarisha huduma za afya nchini .

“Ushirikishwaji kwa jamii katika faida za Bima ya Afya Wote ni muhimu watumishi sekta ya afya na wadau kuendelea kutoa elimu hii kwani Bima ya afya kwa wote itahakikisha kila Mtanzania anapata matibabu kila kujali kipato chake hali itakayosaidia kupata matokeo mazuri kuboresha huduma za afya kwa mwananchi,” amesema Mabwe.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kitaalam  ya ushauri wa  Mpango wa Taifa wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii (CBHP-TAC Meeting),  wakishiriki kwenye kikao chenye lengo la uimarishaji afua za huduma za afya ngazi ya jamii  kilichoratibiwa na  Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo PACT   -Tanzania na BMF.

Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, unatarajiwa kusomwa Bungeni hivi karibuni na ukipitishwa utaanza kufanya kazi rasmi Mwezi Julai, 2023 na itarahisisha ubora wa huduma na kila mwananchi kuwa na uhakika wa kupata matibabu.

HakiElimu wataka hatua zaidi kukomesha viboko Shuleni
Wahimizwa kuripoti Habari za uibuaji Viongozi Wanawake