Sakata la Kiwanda cha Saruji cha Dangote kusitisha uzalishaji wa bidhaa hiyo limeendelea kuwa gumzo baada ya kubainisha kuwa Serikali imekubaliana na kampuni hiyo kuiuzia gesi asilia kwa dola za Marekani 5.14 kwa futi za ujazo 1,000 kuanzia Januari mwakani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage Jijini Dar es salaam,ambapo amesema wameshauriana na Dangote kuwa anapotumia diezel anapata hasara na akitumia gesi asilia kwa kuuziwa kwa dola 5.4 ni nafuu kwa uzalishaji wa kiwanda chake.
“Sitaki kiwanda hata kimoja kipotee, hasara za kutoa nishati bure ni kubwa sana, tuna viwanda vya saruji 10, kama mlezi wa wana viwanda siwezi kumpa mmoja bure na wengine niwauzie, namsihi anayetaka kwenda kununua gesi aua makaa ya mawe aende akanunue”.amesema Mwijage
Aidha Serikali imesema, haitakubali kuona mwekezaji anaondoka nchini kwa sababu ya vikwazo ambavyo vinaweza kushughulikiwa kwakuwa lengo lake ni kuongeza wawekezaji na si kuwafukuza.