Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa serikali imepanga kununua ndege zingine 4, mbili za masafa marefu na mbili za masafa ya kati, ambazo zitawarahisishia wafanyabiashara wa bidhaa zinazoharibika haraka kusafirisha bidhaa zao kwa uharaka.

Majaliwa amesema hayo leo Desemba 5, 2020, wakati wa uzinduzi wa kongamano la uwekezaji na biashara ya mazao ya bustani, na kuongeza kuwa bidhaa kama minofu ya samaki, mazao ya bustani na nyama yanahitaji kuwa na uhakika wa usafiri.

“Pamoja na Ndege ya mizigo, serikali itanunua Ndege kubwa 2 za masafa marefu na 2 za masafa ya kati ili kuongeza fursa za kibiashara zaidi, pia imeshaunda kamati maalum kwa ajili ya kuainisha changamoto za usafirishaji na kimfumo katika bandari na viwanja vya ndege ili kufanya maboresha yanayohitajika,” amesema Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amebainisha kuwa kwa kutambua uwepo wa changamoto katika usafirishaji wa bidhaa, kupitia ilani ya CCM Serikali imeweka bayana mpango wa kuboresha mazingira ya usafirishaji wa bidhaa zinazoharibika kwa haraka, kwa kununua ndege ya mizigo kwa kuzingatia mahitaji ya biashara na ukuaji wa uchumi nchini.

Magufuli ateua Baraza jipya la Mawaziri, Naibu Mawaziri
Ivory Coast: Gbagbo arudishiwa hati za usafiri