Serikali imesema kuwa ina mpango wa kuongeza fedha katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ili kuongeza idadi ya wananchi watakaonufaika na mradi huo.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika wakati wa maswali na majibu

Amesema kuwa malengo ya TASAF ni kufikia walengwa wote ambapo hadi sasa asilimia 70 ya walengwa wamefikiwa na mradi huo, hivyo serikali imedhamiria kuongeza fedha.

“Malengo ya TASAF ni kufikia walengwa wote wanaokubali kusaidiwa, mpaka sasa tumefikia walengwa asilimia 70. TASAF kwenye awamu ya tatu B, malengo ya serikali ni kufikia walengwa wote na ili tuwafikie walengwa wote lazima serikali iongeze fedha,” amesema Mkuchika.

Aidha, Waziri Mkuchika ameahidi kufanyia kazi changamoto zinazoikabili mradi huo ikiwemo malalamiko ya upendeleo katika utolewaji wa fedha hizo.

Hata hivyo, Mradi wa TASAF ulianza rasmi mwaka 2013 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2023 ambapo unatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi mfululizo ambapo vimegawanyika kwa awamu mbili. fedha za utekelezaji wa mradi huo ni za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB)

Geoffrey Kondogbia, Frederic Nimani ruhsa kucheza Afrika ya kati
Abdoul 'Razza' Camara aombwa kustaafu soka

Comments

comments