Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulenga, amebainisha kuwa nivyema shughuli za uvuvi zikarasimishwa ili wavuvi waweze kunufaika kupitia sekta hiyo kwa kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha pamoja na kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Ulenga ameyasema hayo alipokuwa kwenye ziara yake Mkoani Kagera wakati wa kikao na wawakilishi kutoka katika taasisi za kifedha, mifuko ya hifadhi za jamii, pamoja na baadhi ya wavuvi wa wilaya hiyo.

Amesema sekta ya uvuvi nchini zikiwemo shughuli zinazofanywa kwenye ziwa Victoria bado hazijatoa mchango wa kutosha katika pato la Taifa.

“Jumla ya thamani ya biashara ya mazao ya samaki kwa mwaka mmoja kwa ziwa Victoria katika nchi ya Tanzania, Kenya, na Uganda inakadiriwa kuwa sh. Tirioni 6, Tanzania inapata Tirioni 1.6, wakati inamiliki eneo kubwa la ziwa, Uganda na Kenya zinazomiliki eneo dogo zinapata Tirioni 4.4., tafsiri yake nikwamba bado hatujanufaika vya kutosha na ziwa victoria” amesema Ulenga.

Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Ulenga, ametaka shughuli za uvuvi zirasimishwe na wavuvi waweze kupata mikopo ili kukuza sekta hiyo ambayo imekuwa ikitegemewa katika kuchangia pato la Taifa na mtu mmoja mmoja.

Naibu Waziri Ulenga, ameendelea na ziara yake mkoani humo ambapo tayari ametembelea kijiji cha Mlela kilichopo kata ya Kishanda na kutoa ahadi ya shilingi milioni Mbili kukarabati josho la kijiji hicho, pamoja na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa anakusanya mapato ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Wachezaji Spurs wamkasirisha Mauricio Pochettino
Chris Brown kuwa 'Bestman' harusi ya Davido