Waziri wa Katiba na Sheria Dokta Mwigulu Nchemba ameagiza taarifa zote za wananchi ambazo zimesajiliwa katika mfumo wa serikali kurasimishwa ili kusaidia kuwaondolea usumbufu wananchi kujisajili mara kwa mara.

Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo Desemba 21, 2020 wakati akizungumza na watumishi wa taasisi hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Jijini Dar es salaam.

Nchemba amesema ni vyema taarifa ambazo tayari zimeshatambulika na kufanyiwa kazi na serikali zikatumika.

“Kwa sababu serikali ni moja kuna taarifa nyingi tayari zimeshafanyiwa kazi na kutambulika rasmi kuwa ni taarifa za serikali, ni vyema tukaendelea kuzitumia kwa kuwa vyanzo vyake ni serikali,” amesema Nchemba.

Pia Nchemba amemuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa RITA pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA kuhakikisha kuwa wanaweka mkazo kuhakikisha taasisi hiyo inahamia Dodoma haraka iwezekanavyo.

Waziri Mkuu apigia chapuo sekta binafsi
KMC FC mguu sawa kuikabili JKT TANZANIA