Serikali imeahidi kuvisimamia vituo vyote vya redio na televisheni nchini kuhakikisha vinacheza kwa kiwango kikubwa zaidi muziki wa nyumbani zaidi ya muziki wa nje.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nauye aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa kuanzia Januari Mosi mwaka 2016 watasimamia sheria na kuhakikisha kila msanii analipwa mrabaha kutokana na nyimbo zake kupigwa kwenye vituo vya redio na runinga nchini.

“Mimi nataka watu waniamini historia yangu, waamini watu watalipwa na haki yao wataipata na jasho lao watalipata. Nilichowaambia kila jambo jipya lazima litakuwa na mapungufu ila sheria ndio zitatuongoza, kila redio na TV zenye vipindi vya burudani wanatakiwa kuhakikisha 60% ya content wanayoitoa iwe ya nyumbani, hakuna wakukwepa hili,” alisema.

Nape alisema kuwa tayari serikali imeshakaa na wamiliki wa vyombo vya habari na kukubaliana kuhusu utaratibu utakaotumika kuwalipa wasanii mirabaha kutokana na nyimbo zao kuchezwa.

Picha: Mtindo Huu wa 'Kuotesha' Mmea Kichwani Unatajwa kufunika Mwaka 2015
Samatta Asaka Baraka Za Serikali Kabla Ya Kwenda Nigeria