Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Amani Chande amesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Mto Msimbazi utaanza mara baada ya serikali kuidhinisha kuhusu matumizi ya fedha za mkopo kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.

Amesema hayo leo Aprili 29, 2021 bungeni jijini Dodoma wakati, akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Abbas Tarimba aliyehoji ni lini serikali itaanza ujenzi wa Mto Msimbazi ambao umeainishwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020 – 2025.

Chande amesema kuwa Serikali imepanga kulibadili eneo la bonde la mto Msimbazi kuwa eneo la uwekezaji na fursa mbalimbali, na mpaka sasa usanifu wa mradi huo umekamilika.

Aidha Chande amesema kuwa ilikuhakikisha athari zinazojitokeza wakati wa mafuriko zinapungua wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wanakifanyia usafi wa mara kwa mara kipande cha Mto Msimbazi cha daraja la Jangwani.

Halmashauri kuu ya CCM Taifa yaketi, uchaguzi wawadia
Waziri Mkenda awaonya jeshi la polisi