Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wananchi waelewe dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Mji Mkongwe unabaki kama ulivyokuwa miaka 200 iliyopita na si kuubadilisha.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo akiwa Shangani hii leo tarehe 22 Machi 2023 wakati akizindua jengo jipya la Tembo Mkoa wa Mjini Magharibi na kuongeza kuwa wapo wanaojaribu kupotosha kuwa Serikali ina lengo la kuubadilisha Mji Mkongwe kwa kuugawa na kubinafsisha taarifa ambazo si sahihi.

Amesema, “lengo ni kuwapa watu wenye uwezo kuyajenga majengo hayo , kuyatunza ili yaweze kudumu miaka mia mbili ijayo kwa mfano Jengo la sasa la Tembo Hoteli lilikuwa Ubalozi wa Marekani mwaka 1831 na Jengo lililozinduliwa kwa marekebisho ilikuwa ni Skuli mwaka 1944.”

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia amewakaribisha wawekezaji waje kushirikiana na Serikali kurudisha hadhi ya Mji Mkongwe na kuujenga huku akitoa miezi mitatu kwa waliopewa Majengo mbalimbali kwa ajili ya kuyarekebisha na kuyaendeleza wakishindwa Serikali itayachukua .

Ameongeza kuwa, Serikali imeamua kutenga fedha kuhakikisha inaleta mfumo bora wa maji, mfumo wa kisasa wa umeme, huduma ya Internet, ujenzi wa barabara katika Mji Mkongwe ili kuwa kivutio kwa utalii kumshukuru Mfalme wa Oman, Sultan Haitham Bin Tariq M. Said na Serikali yake kwa msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 21 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Beit-al-Ajaib.

Meridianbet Kasino ya Mtandaoni Yaja na kitu kipya
Wiki ya Maji: Wahimizana kuyatumia kwa unyenyekevu