Leo Ijumaa Februari 2, 2018 Katika kikao cha Nne Mkutano wa Kumi wa Bunge, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Serikali ya Awamu ya Tano, Ummy Mwalimu ameongelea bungeni ujio wa tiba mbadala wa tatizo la Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

Ambapo amesema kuwa tatizo hilo ni kubwa sana na linalowasumbua wanawake wengi.

Hivyo amesema serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa Kizazi kwa wasichana wadogo.

Na kueleza kuwa chanjo hiyo itatolewa kwa wasichana kuanzia miaka 14 ambao hawajawahi kujamiana.

Pia ameongezea kuwa wanaume wengi hawapimi saratani ya tezi dume, kwa kuogopa kipimo, hivyo amewashauri wanaume kupima ugonjwa huo kwani siku hizi umekuwa kama ugonjwa wa Taifa ili kuepukanana adha ya matibabu katika hatua mbaya ya ugonjwa huo.

 

Sirro atoa maagizo mazito
Breaking News: Wahamiaji haramu 90, wahofia kufa maji