Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 4.6 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa katika ranchi ya Kongwa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mbegu bora za ng’ombe, uchimbaji wa visima na ununuzi wa matrekta.

Hayo yameainishwa na Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu wakati akisoma taarifa ya utendaji wa shamba la mifugo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shamba la mifugo la NARCO – Kongwa ili kujionea maendeleo ya shamba na shughuli za ufugaji.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Daniel Elias Mushi (kulia) naMeneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Elisa Binamungu wakikagua na maeneo ya Ranchi hiyo, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kufanya ziara ya kikazi katika ranchi hiyo hivi karibuni.

Amesema Serikali imeongeza uzalishaji wa nyama ya ng’ombe, ambapo ranchi ina ukubwa wa hekta 38,000 zenye uwezo wa kuweka uniti za mifugo 25,000 na kwamba eneo la Kongwa lipo kimkakati hivyo menejimenti ya shamba hilo itumie fursa hiyo kuuza bidhaa zake na kujitangaza ili waweze kunufaika na uwepo wa barabara kuu..

“Eneo hili limegawanywa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ina jumla ya uniti za mifugo 12,427 na sehemu ya pili ina uniti za mifugo 16,897 na sisi tuna mifugo mingi sana ila mazao haya ya mifugo na nyama hayauziki nje kwa kiasi kikubwa,” amesema Binamungu.

Uhalifu: Polisi yanasa Bastola, wahalifu wakimbia
Watu 60 wawekea puto, mmoja atolewa - Pro Janabi