Serikali imesema kuwa imepunguza muda wa masomo kwa madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kutoka miaka 13 mpaka sita, ili kuongeza idadi ya wataalamu nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tiba kutoka MOI, Dkt. Samuel Swai amapo amesema kuwa Tanzania ina madaktari bingwa 10 katika kitengo cha mifupa (MOI) wawili wengine wanatoa huduma Hospitali ya Bugando Mwanza.

“Idadi ya madaktari bingwa waliobobea katika upasuaji ubongo ni ndogo ikilinganishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa dharura hasa wa ajali, tunapokea kwa siku watatu mpaka watano wanaohitaji upasuaji,” amesema Dkt. Swai

Amesema kuwa kutokana na uhaba huo wa wataalamu, waliomba kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na hivi sasa tayari wameanza kutoa mafunzo kwa muda wa miaka sita.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Weill Cornell, New York Marekani, Dkt. Roger Hartl amesema kuwa kwa ushirikiano wa miaka 10, Kitengo cha Mifupa MOI kimeboresha matibabu kwa nchi ya Tanzania

NEC yaruhusu leseni ya udereva kupigia kura
Anthony Joshua kuzipiga na Carlos Takam