Waziri wa Ulinzi nchini Kenya, Mkuu wa Polisi pamoja na Afisa Mkuu kutoka Idara ya Uhamiaji wameagizwa kuripoti mahakamani.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya serikali kukaidi maagizo yaliyotolewa na Mahakama Kuu nchini humo juu ya kumwachilia huru wakili wa upinzani, Miguna Miguna na kumfikisha mahakamani hii leo.

Aidha, ni siku ya pili sasa kwa Miguna kukesha katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, tangu wakili huyo alipowasili nchini Kenya kutoka Canada siku ya Jumatatu.

Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada ya kudaiwa kutowasilisha hati ya kusafiria ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Hata hivyo, Miguna alitimuliwa kwenda nchini Canada mwezi Februari baada ya kumuapisha kiongozi wa upinzani,  Raila Odinga alipokuwa anajiapisha kuwa ‘Rais wa Wananchi’

Wanasiasa Kenya wagoma kukalia viti vya plastiki
Lema: Viongozi wa Chadema tunavumilia mateso mengi