Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa Serikali haijazuia maudhui  ya redio za nje kusikika nchini bali imeagiza maudhui  hayo yapate kibali kutoka  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ndio inayosimamia maudhui ya utangazaji nchini.

Ameyasema hayo katika mahojiano na redio Mashujaa FM ya mkoani Lindi ambapo amesema redio za nje zinapaswa kuitaarifu TCRA maudhui inayotaka kurusha, lengo likiwa ni kulinda na kuheshimu maadili ya nchi.

“Serikali haijakataza redio za ndani kujiunga au kupokea maudhui kutoka redio na televisheni za nje bali kinachotakiwa kufanyika ni kufuata utaratibu ambao Serikali imeweka,Nchi yetu sio ya kupokea na kutoa kila kitu tayari ni nchi huru hivyo lazima iheshimiwe”,amesema Waziri Mwakyembe.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe amewataka waandishi wa habari katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika kampeni na hatimaye Uchaguzi Mkuu Agosti 28, 2020 watumie kalamu zao vizuri kwa kuandika na kutangaza habari zenye ukweli, uwazi, na zilizochakatwa vizuri ambazo hazionyeshi upendeleo wowote kama ambavyo taaluma ya habari inataka.

Mazingiza akabidhi ofisi Simba SC
Manara awapa onyo TFF, amtaja Rais Magufuli